Klabu ya Simba sc imefanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la Mapinduzi inayoendelea visiwani Zanzibar baada ya kuifunga Singida Fountain Gate Fc kwa mabao 2-0 katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Amani Visiwani humo.
Simba sc ilipata mabao hayo kupitia faulo ya Andre Onana dakika chache tangu kuanza kwa kipindi cha pili ambapo kipa wa Singida FG Ibrahim Parapanda alishindwa kuiona faulo hiyo iliyopigwa kiufundi wa hali ya juu huku baada ya kuingia kwa bao hilo Simba sc waliongeza spidi ya kushambulia na dakika ya 56 Luis Miqquisone alifunga bao la pili kwa shuti kali akimalizia kazi ya Shomari Kapombe.
Licha ya kubakiza mchezo dhidi ya APR ya Rwanda, Simba tayari imejihakikishia kucheza robo, huku ikijikusanyia alama sita na mabao matano katika michezo miwili ya kundi hilo ambapo kipigo hicho kwa Singida FG ni muendelezo wa ubabe kwa timu hiyo kuanzia katika ligi kuu ya Nbc.
Katika mchezo huo kiungo wa Simba sc Fabrice Ngoma aliibuka kuwa mchezaji bora wa mchezo huo huku beki wa Singida FG Kelvin Kijiri akiibuka kuwa mchezaji mwenye nidhamu ambapo wote wawili walipata zawadi za kiasi cha fedha.
Hicho ni kipigo cha tatu kwa Singida mbele ya Simba kwa msimu huu, baada ya awali kufungwa kwa penalti 4-2 kwenye Ngao ya Jamii na 2-1 katika Ligi Kuu Bara.