Connect with us

Soka

Simba sc Yatinga Klabu Bora Afrika

Takwimu zilizotolewa na Shirikisho la soka barani Afrika (Caf) imeonyesha kuwa klabu ya Simba sc ni miongoni mwa klabu arobaini bora barani Afrika ikishika nafasi ya 16  kati ya 40 zilizotajwa katika orodha hiyo.

Katika orodha hiyo klabu ya Al ahly ya nchini Misri inashika nafasi ya kwanza huku Esparance ya Tunisia ikishika nafasi ya pili na Wydad Casablanca anayochezea Mtanzania Simon Msuva inashika nafasi ya tatu kwa ubora na majirani zao wa Raja Casablanca wakishika nafasi ya nne na tano bora ikifungwa na Mamelod Sundowns ya Afrika kusini.

Simba sc imeshika nafasi ya 16 na ikiwa ya kwanza kwa upande wa Afrika Mashariki na kati ikifuatiwa na Fc Platnumz ya Zimbambwe ambapo kwa Afrika ipo nafasi ya 21 na ya pili kwa ukanda wa Afrika Mashariki na kati.

Mafanikio hayo kwa klabu ya Simba sc yamechangiwa na kufanya vizuri kwa misimu miwili mfululizo katika michuano ya klabu bingwa barani Afrika na kufanikiwa kuingia hatua ya nane bora kwa msimu huu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka