Connect with us

Soka

Simba Sc Yapigwa Misri

Kama yalivyokua matarajio ya wengi kwamba klabu ya Simba sc itapoteza mchezo wale wa hatua ya robo fainali dhidi ya Al Ahly Fc uliofanyika nchini Misri katika uwanja wa Cairo Internation ambapo Simba sc ilikubali kipigo cha mabao 2-0.

Katika mchezo wa awali machi 29 jijini Dar es salaam timu hiyo ilikubali kipigo cha 1-0 ambapo ilikua na mlima mrefu wa kupanda katika mchezo wa marudiano nchini Misri ikiilazimu kushinda kuanzi mabao mawili kuendelea ndio ifuzu kuelekea nusu fainali.

Simba sc licha ya kumiliki mpira ilikubali mabao ya dakika ya 47 ya Amri El Solia na dakika ya 90+9 kutoka kwa Mahmoud Kahraba na kuufanya mchezo huo jumla kufungwa kwa mabao 3-0 katika michezo yote miwili ya nyumbani na ugenini.

Kutokana na ushindi huo sasa Al Ahly itasubiri mshindi katika ya Tp Mazembe dhidi ya Petro de Luanda ili kujua itakutana na nani katika hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka