Connect with us

Soka

Simba Sc Yapata Mrithi wa Inonga

Klabu ya Simba sc inamtolea macho mlinzi wa ASEC Mimosas Anthony Tra Bi Tra kujiunga na timu hiyo kwa ajili ya kwenda kuziba pengo la Henock Inonga Baka ambae taarifa za ndani  zinaeleza kuwa mwishoni mwa msimu anaelekea AS FAR Rabat ya Morocco.

Nyota huyo raia wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 25 ameiongoza klabu yake ya Asec Mimosas kutinga hatua ya robo fainali ya CAF Champions League msimu huu akicheza michezo yote 12 ya ambayo klabu yake wamecheza kwenye michuano hiyo.

Inaelezwa kuwa Anthony Tra Bi anataka kuondoka ndani ya kikosi hicho mwishoni mwa msimu huu na anataka kwenda kutafuta changamoto baada ya kuitumikia timu hiyo toka mwaka 2021.

Simba sc sasa suala hilo linabaki mikononi mwao kama klabu kutokana na ukweli kwamba Asec siyo wachoyo linapokuja suala la kuuza mchezaji hasa ambaye anafanya vizuri katika kikosi chao.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka