Connect with us

Soka

Simba Sc Yalamba Udhamini 1.5b

Klabu ya Simba sc imefanikiwa kuingia makubaliano na kampuni ya bia ya Serengeti ya udhamini kupitia kinywaji cha Prisner Lager kwa muda wa miaka mitatu wenye thamani ya pesa za kitanzania shilingi bilioni moja na nusu.

Katika udhamini huo kampuni hiyo itatumia nembo na picha za wachezaji wa klabu hiyo katika matangazo yake ambapo itafaidika na kupanda kwa mauzo huku Simba sc itafaidika na fedha hizo katika uendeshaji wa klabu hiyo.

Katika hafla hiyo klabu ya Simba sc iliwakishwa na Afisa Mtendaji mkuu wa klabu hiyo Iman Kajula pamoja na wajumbe wa bodi ya klabu hiyo Asha Baraka na Raphael Chegeni.

“Hili ni tukio la kihistoria. Katika mechi zote ambazo Simba inacheza mtaani kunanona na naamini Pilsner Lager kuwa mshirika wa Simba hata mauzo yataongezeka. Mashabiki wa Simba wanapenda kujipa raha. Tunaamini ushirikiano huu utazidi kutujenga. Tunawaahidi kupitia Simba bia itakuwa maarufu zaidi.” Alisema mjumbe wa Bodi, Raphael Chegeni

Kwa upande wa kampuni ya bia ya Serengeti yenyewe mbali na Mkurugenzi wa Masoko Anitha Rwehumbiza,Pia iliwakilishwa na mkurugenzi mtendaji Obinna Anyalebechi ambaye alisema kuwa “Tunajivunia kuziunganisha taasisi mbili kubwa za SBL na Simba kwa mkataba wa udhamini wa miaka mitatu. Kupitia udhamini huu utaifanya bia yetu ya Pilsner Lager kuwa mdhamini wa Simba.”

“Udhamini huu utakuwa na thamani ya Tsh. 1.5 bilioni. Kwa udhamini huu tunaamini utasaidia kukuza michezo nchini kwetu. Simama Imara, Songa Mbele Kama Simba.Alisema Obinna.
Imani Kajula ambaye ni Mtendaji mkuu wa Simba sc alisema kuwa fedha hizo zitasaidia uendeshaji wa klabu wa kila siku ambao kwa kawaida unahitaji kiasi cha fedha hasa kulipa mishahara na kuendeleza miradi mbalimbali ya klabu.
“Ni ubia wa nguvu kabisa, ubia wa Simba wawili. Hii ni package ambayo imekuja wakati mwafaka. Serengeti ni mbia mkubwa sana wa mpira wa Tanzania, huu ni mwendelezo wa kusaidia mpira.”Alisema Iman
“Udhamini huu utasaidia uendeshaji wa klabu, gharama za uendeshaji wa vilabu huwa ni kubwa. Upatikanaji wa fedha ni muhimu sana. Tunawashukuru kukubali kuungana nasi kama wadhamini wa Simba.”
Simba sc imekua na mafanikio ndani ya uwanja kiasi cha kuvuna mashabiki wengi kwa miaka ya hivi karibuni na mashabiki hao huvutia wawekezaji ambapo mpaka sasa imefanikiwa kupata udhamini wa makampuni kama M-bet,Metl,Africarriers na mengineyo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka