Connect with us

Soka

Simba sc Yailaza Prisons 1-0

Klabu ya Simba sc imefanikiwa kuibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa ligi kuu nchini uliofanyika katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam.

Simba sc ilianza na kikosi ikiwapumzisha Jonas Mkude na Sadio Kanoute ambao nafasi zao zilichukuliwa na Erasto Nyoni na Mzamiru Yassin huku eneo la ushambuliaji likiwa na Cletous Chama,Hassan Dilunga,Rally Bwallya na Meddie Kagere ambao walibanwa vilivyo na mabeki wa Prisons kiasi cha kusababisha mapumziko kwenda wakiwa hawajafungana wala Simba sc kupiga shuti lililolenga lango.

Kipindi cha pili licha ya Simba sc kufanya mabadiliko kuwaingiza John Bocco,Pape Sakho na Jimson Mwinuke bado Prisons walijitahidi kuzuia kwa mipango na kushambulia kwa kushtukiza mpaka mwamuzi alipoamuru pigo la penati katika mpira ambao beki wa Prisons hakuunawa na Meddie Kagere kufunga.

Sasa Simba sc imefikisha alama 28 ikiwa na mechi 14 huku ikitarajiwa kucheza na Mbeya Kwanza siku ya Jumamosi Februari 5 katika uwanja huo huo kabla ya kuhamia katika michuano ya kimataifa.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka