Connect with us

Makala

Simba Sc Yaachana na Chilunda

Klabu ya Simba imeachana na mshambuliaji wake Shaaban Idd Chilunda baada ya kudumu kwa msimu mmoja pekee ambapo pia katikati ya msimu alitolewa kwa mkopo KMC alipomalizia msimu huu wa ligi kuu nchini.

Chilunda alisajiliwa na Simba sc baada ya kumaliza mkataba wake na klabu ya Azam Fc ambapo tangu asajiliwe klabuni hapo amekua na nafasi finyu ya kucheza mbele ya Jean Baleke,John Bocco na Moses Phiri kipindi wapo Simba sc hali iliyosababisha atolewe kwa mkopo Kmc wakati wa dirisha dogo la usajili mwezi Januari.

Mchana huu klabu hiyo imetoa taarifa rasmi kuachana na staa huyo akiwa ni mchezaji wa tatu kutemwa baada ya John Bocco na Saido Ntibanzokiza huku jioni ya leo klabu hiyo itatoa taarifa ya kuachana na staa mwingine ambapo mpaka sasa waliopo kingaangoni kuhusu hatma zao ni pamoja na Pa omar Jobe, Fredy Michael,Abdalah Hamis,Sadio Kanoute,Kennedy Juma na makipa Aishi Manula ama Ayoub Lakred ambao wanatajwa kuwa na ofa nono nje ya Simba sc.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala