Connect with us

Soka

Simba Sc Waifunga Tembo Fc

Timu ya Simba sc imefanikiwa kuingia hatua ya 32 bora ya michuano ya kombe la Shirikisho la Azam baada ya kufanikiwa kuifunga timu ya Tembo Fc mabao 4-0 katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Chamazi jijini Dar es salaam.

Simba sc ikianza na mastaa wengi wageni sambamba na wale ambao huwa hawapati nafasi mara kwa mara huku ikichanganya na mastaa wa kikosi cha kwanza kama Sadio Kanoute na Saido Ntibanzokiza walipata bao la kwanza kupitia kwa Luis Miqquisone dakika ya 11 huku Saido Ntibanzokiza akiongeza la pili dakika ya 31.

Kipindi cha pili Simba sc waliongeza mabao mawili kupitia kwa Salehe Karabaka dakika ya 81 na usajili mpya Pa Omar Jobe alifunga bao la mwisho dakika ya 83 ya mchezo na kuivusha Simba sc katika hatua inayofuatia.

Timu zingine zilizofuzu hatua hiyo kutoka ligi kuu ya Nbc ni pamoja na Yanga sc,Azam Fc,Mtibwa Sugar na zingine mbalimbali pamoja na timu za ligi ya Championship ambayo ni ligi ya daraja la kwanza nchini.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka