Connect with us

Soka

Simba Sc Vs Yanga Sc Mechi ya Kisasi

Kesho Aprili 20 macho ya watanzania yatakua katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam ambapo kutakua na mchezo baina ya watani wa Jadi Simba sc dhidi ya Yanga sc kuanzia majira ya saa kumi na moja jioni.

Mchezo huo tayari umekua gumzo nchini kutokana na ukweli kwamba huwa hautabiri huku ukitarajiwa matokeo yatakayopatikana ndio yatatoa dira ya ubingwa wa ligi kuu hapa nchini msimu huu kutokana na timu hizo kuzudiana alama sita ambapo Yanga sc ana alama 55 na Simba sc ana alama 46 akiwa na mchezo mmoja mkononi ambao akishinda atapunguza pengo la alama mpaka sita na akiifunga Yanga sc kesho atakua anadaiwa alama tatu pekee.

Yanga sc wao endapo wakishinda watakua moja kwa moja wamejihakikishia asilimia kubwa ya kutwaa ubingwa kwani wataiacha Simba sc alama 12 huku Azam Fc ikiachwa alama saba na ikiwa imezidi kwa michezo mmoja zaidi.

Makocha wa timu zote mbili wanatambua presha ya mchezo huo kutoka kwa viongozi na mashabiki wa vilabu hivyo huku Simba sc wakiwa na presha kutokana na ukweli kuwa timu hiyo haiko vizuri na wana deni la kufungwa mabao 5-1 katika mchezo uliopita.

“Mashabiki wetu wamekuwa nyuma yetu wakati wote, hata dakika ambazo hatuchezi vizuri Uwanjani wamekuwa wakiendelea kushangilia kwa nguvu na kutupa nguvu.Nina amini kesho kutakuwa na namba kubwa ya mashabiki wetu Uwanjani na tumejiandaa kwa mchezo mzuri” Alisema kocha Miguel Gamondi wa Yanga sc
“Simba SC ni timu nzuri, nasi tuna timu nzuri, bila shaka utakuwa mchezo mzuri wenye ushindani hivyo tumejiandaa vyema sana kuhakikisha tunaondoka na alama tatu muhimu” Alisema beki Dickson Job akiongea na waandishi wa habari kuhusu mchezo huo.
Kwa upande wa Simba sc kocha Seleman Matola alisema kuwa mchezo huo hautabiriki japo Yanga sc wapo vizuri uwanjani “hii ni mechi mpya na yenye mbinu tofauti na tuna wachezaji wengi wa kucheza mechi hizi hivyo tumewaandaa vizuri kuhakisha wanakua bora.
Yanga sc na Simba sc kwa siku za hivi karibuni zimezidi kuvuna mashabiki wengi huku zikifanya vizuri kimataifa kiasi cha Tanzania sasa kuanza kuingiza timu mbili katika michuano ya Caf.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka