Simba SC imetinga hatua ya fainali Mapinduzi Cup 2022 baada ya kuifunga Singida Fountain Gate kwa penalti 3-2 baada ya kumaliza dakika 90 matokeo yakiwa 1-1 katika mchezo wa hatua ya nusu fainali uliofanyika katika uwanja wa Amani Visiwani Zanzibar na kuhuduriwa na mashabiki lukuki wa soka visiwani humo.
Singida Fountain Gate Fc ilianza kupata bao kupitia kwa Elvis Rupia dakika za mapema kipindi cha kwanza akiiunganisha pasi ya Mouruf Tchakei aliyeinasa pasi ya Kennedy Juma dakika ya 11 ya mchezo na Simba ikasawazisha dakika za mwishoni baada ya zile za nyongeza kumalizika likifungwa na Fabrice Ngoma.
Katika mikwaju ya penalti Meddie Kagere aliyekuwa na nafasi ya kurudisha matumaini Singida Fountan Gate ambao walilazimika kusawazisha makosa baada ya kukosa penalti mbili na matokeo kuwa 3-2 ambapo staa huyo wa zamani wa Simba sc alikosa penalti ya mwisho na kufanya Simba kuwa mshindi.
Simba itacheza fainali dhidi ya Mlandege FC Januari 13 katika uwanja huo huo wa amani ambapo Simba sc anapewa nafasi kubwa ya kuibuka mabingwa wa michuano hiyo na kunyakua kiasi cha Tsh 100 milioni za zawadi kwa mabingwa wa michuano hiyo.
Katika mchezo huo beki Kelvin Kijiri aliibuka kuwa mchezaji bora wa mechi na kufanikiwa kujinyakulia zawadi ya fedha taslimu kiasi cha shilingi milioni moja za kitanzania.