Connect with us

Makala

Simba queens Yaachana na Mgundaa

Klabu ya Simba queens imeachana na kocha wake mkuu Juma Mgunda kutokana na kocha huyo kumaliza mkataba wake klabuni hapo.

Mgunda aliyeajiriwa kama kocha msaidizi wa timu ya wanaume akitokea Coastal Union lakini baadae iliilazimu klabu hiyo kumuhamishia timu ya wanawake ya klabu hiyo huku wakiajiriwa makocha wa kigeni katika timu ya wanaume.

Mara kadhaa Mgunda amekua akitumika kama kiraka wa timu ya wanaume ya Simba Sc pindi inapokua imetimua makocha wa kigeni na ikiwa inajipanga kutafuta kocha mpya.

Taarifa iliyotolewa na klabu hiyo inasema kuwa imefikia makubaliano ya kuachana na kocha huyo kutokana na mkataba wake kuisha huku kwa sasa majukumu yake akiachiwa kocha msaidizi Mussa Mgosi.

Simba queens ambayo imefanya vibaya katika michuano ya ukanda wa cecafa kwa wanawake ikishindwa kutwaa kombe hilo katika michuano iliyomalizika hivi karibuni na hiyo ndiyo sababu kuu ya kutoengezewa mkataba kocha huyo.

Mgunda pamoja na kuondoka Simba queens hatarajiwi kama atakaa muda mrefu bila klabu kutokana na kuwa na wasifu mkubwa kwa makocha wazawa huku kwa sasa akiwa ni moja ya makocha wanaoinoa timu ya Taifa ya Tanzania.

Klabu ya Namungo Fc inasemekana imekua ikimtolea macho Mgunda kuinoa klabu hiyo baada ya kutokua na imani na kocha Mwinyi Zahera.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala