Connect with us

Soka

Simba Kuogelea Noti

Taarifa za ndani kutoka klabu ya Simba Mwekezaji wa klabu ya Simba Bilionea Mohamed  Dewji pamoja na wajumbe wa bodi ya wakurugenzi wamekubaliana kutoa Tsh Milioni 87 za ubingwa kwa wachezaji na benchi la ufundi wagawane pesa hizo.

Pia Mo Dewji amejitolea yeye binafsi kiasi cha Tsh Milioni (200) kwa wachezaji wote & na benchi la ufundi la Simba ikiwa ni zawadi ya kutwaa ubingwa msimu huu.

Aidha, wadhamini wakuu wa klabu ya Simba sc Sportpesa watatoa Tsh Milioni (100) ikiwa ni makubaliano ya kimkataba iwapo watatwaa ubingwa.

Kama haitoshi Fatma Dewji dada wa tajiri billionaire Mo Dewji kupitia udhamini wa Mo energy & Mo halisi watatoa zawadi ya Tsh Milioni (75) Huku wadhamini wa jezi kampuni ya  Uhlsport kampuni inayotengeneza jezi za klabu ya Simba watatoa Tsh Milioni (50) kama zawadi ya kutwaa ubingwa msimu huu.

-Kwa hesabu za haraka haraka licha ya kushika kombe Wachezaji pamoja na benchi la ufundi watapewa jumla ya Tsh Milioni 512+ wagawane.

Cc:Mitandao

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka