Connect with us

Makala

Serikali Yaishukia Simba Sc Uharibifu B/Mkapa

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Habari,Sanaa na Michezo ambayo kwa sasa inaongozwa na Waziri Mh.Pro Paramangamba Kabudi imetoa taarifa rasmi ya kulaani uharibifu wa miundombinu ya uwanja wa Benjamin Mkapa wakati wa mchezo wa kombe la Shirikisho barani Afrika baina ya Simba Sc dhidi ya Sfaxien ya nchini Tunisia.

Katika Mchezo huo mara baada ya Simba Sc kupata bao la pili na mwamuzi kumaliza mpira ziliibuka vurugu ambapo mashabiki wa klabu hiyo ya Sfaxien waliwashambulia mashabiki wa Simba sc sambamba na Marefa wa mchezo huo hali iliyopelekea viti zaidi ya mia mbili kuvunjwa.

Katika taarifa yake kwa umma wizara imeonyesha kusikitishwa na vitendo hivyo huku ukiliagiza Shirikisho la soka nchini kuwashughulikia suala hilo ambapo ukarabati unapaswa kufanyika mara moja.

Uwanja wa Benjamin Mkapa unamilikiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo shughuli za uendeshaji zipo chini ya Wizara hiyo.

Tayari klabu ya Simba Sc imejibu taarifa hiyo ambapo pamoja na yote imeahidi kulishughulikia suala hilo mapema iwezekanavyo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala