Connect with us

Soka

Serikali-Ruksa Mapro 10

Waziri wa mwenye dhamana ya michezo Harrison Mwakyembe ameruhusu usajili wa wachezaji 10 wa kigeni katika timu zinazoshiriki ligi kuu nchini.

Awali Waziri Mwakyembe alitoa tamko linaloashilia kutokubaliana na idadi hiyo ya wachezaji wa kigeni jambo lililozua taharuki miongoni mwa wadau wa soka nchini na kuleta sintofahamu baada ya kuwa baadhi ya timu tayari zilikua na idadi hiyo ya wachezaji wa kigeni zikiwemo Simba na Yanga.

Jana katika mkutano na waandishi wa habari Waziri huyo alitoa msimamo wa serikali kukubaliana na suala hilo japo lazima wachezaji hao wakidhi vigezo ikiwemo suala la kuchezea timu za taifa katika nchi walikotoka pia wawe wametoka katika ligi inayofahamika.

“Hatutaki mchezaji ameibuka tu katika ndondo anakuja kuichezea ligi yetu,tumeridhia wachezaji kumi wa kigeni kwa masharti hayo”alimalizi Mwakyembe.

Tamko hilo la Mheshimiwa Mwakyembe linaweza kuziathiri timu ambazo zimesajili wachezaji wa kigeni ambao hawana nafasi katika timu zao za taifa mana linatarajiwa kuanza kutumika kuanzia msimu ujao.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka