Connect with us

Soka

Samia Achangia Mil.500 Stars

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hassan amechangia jumla ya kiasi cha Tsh.milioni mia tano kwa ajili ya kusaidia timu za Taifa za michezo mbalimbali ambayo zitakua zinashiriki kimataifa.

Timu hizo zinajumuisha timu za Taifa za michezo mbalimbali ikiwemo soka kwa wanawake na wanaume,Kikapu,Riadha,soka la ufukweni,mpira wa walemavu na nyinginezo ambazo zitapata nafasi ya kushiriki michuano hiyo duniani ama barani Afrika.

Katika hafla maalumu ya kuchangia tukio hilo iliyofanyika katika hoteli ya Johari Rotana jijini Dar es salaam ambapo mgeni rasmi alikua na Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Majaliwa Kassim Majaliwa Rais Samia alitoa mchango huo wakati akizungumza kwa njia ya simu.

“Michezo pia ni gharama ndugu zangu. Serikali imejitahidi, tumehamasisha, timu zetu zinasonga mbele lakini tumefika mahala tuna uchache wa bajeti. Wito wangu na ombi langu kwenu Watanzania wenzangu, tuchangie timu zetu ili ziende kuwakilisha jina la Tanzania,”Alisema Rais Samia

Jumla ya zaidi ya shilingi bilioni tatu zilipatikana kutoka kwa wadau mbalimbali walioahidi kuchangia yakiwemo makampuni binafsi,Taasisi za Serikali,Wasanii na watu binafsi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka