Connect with us

Soka

Ronaldo aibeba tena Man Utd usiku wa Ulaya

Mshambuliaji wa Manchester United ameiwezesha tena klabu yake kupata ushindi wa pili mfululizo kwenye michuano ya ligi ya klabu bingwa Ulaya baada ya kufunga bao muhimu kwenye ushindi wa 3-2 dhidi ya Atalanta.

Kwenye mchezo huo uliofanyika katika dimba la Old Trafford Atalanta waliondoka kipindi cha kwanza wakiwa na uongozi wa magoli 2-0 kwa magoli ya Mario Pasalic na Mehdi Demiral.

Man Utd walifanya kazi ya ziada kipindi cha pili kwa kusawazisha kupitia kwa Marcus Rashford dakika ya 53 na Harry Maguire dakika ya 75 kabla ya mfalme wa michuano hiyo Cristiano Ronaldo kufunga bao la ushindi dakika ya 81 akipaa juu na kupigwa kichwa kikali kilichojaa nyavuni.

Kwa ushindi huo mashetani hao wekundu wanaongoza kundi F wakiwa na alama 6 na watarudiano na Atalanta ndani ya wiki mbili zijazo huko Italia.

Matokeo mengine ya michuano hiyo usiku wa jana;

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka