Connect with us

Soka

Richard Anold CEO mpya Man Utd

Klabu ya soka ya Manchester united imetangaza rasmi kuwa Richard Anold atakuwa mtendaji mpya wa klabu kuanzai Februari mosi mwaka huu akichukua nafasi ya Mmarekani Ed Woodward anayemaliza muda wake.

Ed Woodward amekuwa mtendaji mkuu wa Manchester united tangu mwaka 2013 pale alipoondoka mtendaji mwenye mafanikio kwenye klabu David Gil kufuatia kuondoka kwa utawala wa muda mrefu wa kocha kutoka Scotland Sir Alex Frguson.

Richard Anold ni mzaliwa wa Manchester,hivyo ni mtu anayeijua klabu hiyo nje ndani huku pia akiwa na uzoefu wa kuhudumu ndani ya klabu kama mjumbe wa bodi akifanya kazi karibu zaidi na Ed Woodward.

Katikakati ya mwaka uliopita Manchester united ilitangaza kuwa mtendaji wake mkuu Ed Woodward ataondoka madaraka mwishoni mwa mwaka huo,lakini kufuatia kufutwa kazi kwa kocha Ole Gunnar Solskjaer bodi a klabu hiyo iliamua kumuongezea muda kidogo ilim kushughulikia suala zima la upataikanaji wa kocha mpya ndani ya klabu likiwa ni jukumu lake la mwisho.

Anold ana kzai kubwa ya kurejesha hadhi ya timu hiyo uwanjani ambapo imekuwa haifanyi vizuri tangu Woodward achukue wadhifa huo,hivyo mashabiki wa klabu hiyo wanasubiri kuona kama atakuwa mtu sahihi hasa yanpokuja maamuzi ya kisoka kwani nje ya uwanja kichumi bado wameendelea kufanya vizuri.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka