Connect with us

Soka

Refa ashangaza AFCON 2021

Katika hali ya kushangaza mwamuzi wa kati wa Kimataifa wa Zambia mwenye uzoefu mkubwa Janny Sikazwe amefanya maamuzi yaliyowaacha wadau wengi wa soka midomo wazi baada ya kumaliza mpira dakika ya 89 dakika moja kabla ya zile 90 za kisheria.

Tukio hilo alilifanya katika mchezo kati ya Tunisia dhidi ya Mali katika michuano ya AFCON 2021 inayoendelea huko nchini Cameroon hali iliyosababisha malalamiko makubwa kutoka benchi la ufundi la Tunisia waliokuwa nyuma kwa 1-0 na kupoteza mchezo huo.

Licha ya mchezo huo kuwa na matukio mengi kipindi cha pili kama vile penati mbili,mabadiliko mengi ya wachezaji,matumizi ya VAR pamoja na majeraha mengi bado refa huyo hakuongeza dakika yeyote,hivyo kuacha maswali kutoka kwa wadau wengi soka duniani kote waliokuwa wakishuhudia mchezo huo.

Kabla ya kufanya hivyo,Sikazwe tayari alishafanya kosa la kumaliza mchezo dakika ya 85 tu ya mchezo kitu ambacho kiliwashangaza Tunisia ambapo baada ya msaada kutoka kwa mwamuzi wa akiba aliamua mchezo huo uendelee kabla ya kuumaliza tena dakika ya 89.

Baada ya mchezo kumalizika kamishina wa mechi hiyo aliamuru timu hizo zirudi uwanjani kumalizia muda uliobaki kitu ambacho Tunisia walikikataa ingawa Mali walirudi uwanjani na kupewa ushindi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka