Connect with us

Makala

Red Arrows Mabingwa Kagame Cup

Klabu ya Red Arrows ya Zambia imeibuka mabingwa wa michuano ya Kagame Cup iliyokuwa inafanyika nchini Tanzania katika uwanja wa Manispaa ya Kinondoni baada ya kuifunga APR Fc ya nchini Rwanda kwa penati 10-9 baada ya kutoka 1-1 katika dakika 90 za kawaida.

Red Arrows inakuwa timu ya kwanza kutoka nje ya Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kubeba taji hilo tangu michuano hiyo ilipoasisiwa mwaka 1967 ambapo mwamuzi aliamuru dakika 30 za nyongeza baada ya zile 90 za kawaida kumalizika kwa 1-1 ambapo Red Arrow ilianza kupata bao la kutangulia kupitia kwa Ricky Banda aliyetumia mpira kambani dakika ya 63 kabla ya Mamadou Sy kuchomoa bao hilo dakika ya 89.

katika changamoto ya mikwaju ya penati timu zote zilipata penati tano za kwanza ndipo zilipoanza zile za piga nikupige mpaka APR walipokosa penati ya kumi baada ya mpigaji kupaisha na kuifanya klabu yake kuambulia $20,000 (Tshs 53.4m) huku mabingwa Red Arrows wakiondoka na kitita cha $30,000 (Tshs 80m).

Michuano hiyo kwa msimu huu imekosa msisimko baada ya klabu tatu kubwa nchini za Yanga sc,Simba sc na Azam Fc kuamua kutoshiriki michuano hiyo na kuamua kwenda katika kambi maalumu za maandalizi ya msimu mpya nje ya nchi ambapo Simba Sc ipo Misri,Azam Fc ipo Morocco na Yanga sc ipo nchini Afrika ya kusini.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala