Connect with us

Soka

Pacome Aitwa Ivory Coast

Kiungo wa Klabu ya Yanga Sc Pacome ZouZou ameongezwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Ivory Coast kuchukua nafasi ya Ibrahim Sangare, anayeitumikia Klabu ya Nottingham Forest ya Uingereza baada ya mchezaji huyo kupata majeraha siku chache kabla ya kuripoti kambini.

Taarifa iliyotolewa na shirikisho la soka nchini Ivory Coast imeonyesha kuwa mastaa watatu walioitwa awali wametemwa kutokana na majeraha yanayowakabili ambapo Séko Fofana, Ibrahim Sangaré na Evan Ndicka wote wameachwa kutokana na kuwa na majeraha huku nafasi zao zikizibwa na Kader Keita,Pacome Zouzoua na Emmanuel Agbadou.

“Shirikisho la Soka la Ivory Coast linafahamisha waandishi wa habari na umma kwamba wachezaji, Séko Fofana, Ibrahim Sangaré na Evan Ndicka, walioitwa na Kocha Emerse Faé, kwa mechi mbili za kirafiki, Ivory Coast-Benin mnamo Machi 23, 2024 huko Amiens (Ufaransa) na Ivory Coast -Uruguay mnamo Machi 26, 2024 huko Lens (Ufaransa), hawatapatikani kwa sababu za matibabu ya majeraham hivyo kwa madhumuni haya, Séko Fofana (Al-Ettifaq FC) mwenye maumivu amebadilishwa na Kader Keita (CFR Cluj, Romania) na Ibrahim Sangaré, ambaye alijisikia vibaya baada ya mechi na klabu yake ya Nottingham Forest, nafasi yake inachukuliwa na Zouzoua Pacôme (Young Africans SC, Tanzania).” Ilisomeka Taarifa hiyo iliyotolew Shirikisho la soka nchini Ivory Coast.

Pia taarifa hiyo iliendelea kuwa “Emmanuel Agbadou (Reims, Ufaransa) aliitwa kuchukua nafasi ya Evan Ndicka ambaye pia alijisikia vibaya mazoezini”.

Pacome amekua na wakati mzuri tangu ajiunge na Yanga sc akitokea Asec Mimosa ya nchini kwa Ivory Coast ambapo mpaka sasa amefunga jumla ya mabao saba katika ligi kuu nchini huku akiisaidia klabu yake ya Yanga sc kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka