Connect with us

Soka

OLE BADO YUPO SANA OLD TRAFFORD

Uongozi na vigogo wa Man Utd ukiongozwa na Sir Alex Ferguson umempa nafasi ya mwisho mkufunzi wa timu hiyo Ole kuiongoza katika michezo kadhaa ijayo.
(chanzo:skysports)

Solskjaer anazidi kuwa kwenye presha ya kuendelea kuwepo Old Trafford na amepewa mchezo wa Jumamosi dhidi ya Tottenham Hotspurs kujaribu kubadili hali ya hewa na kutetea kibarua chake.

Man Utd imekusanya alama moja tu kati ya michezo mitano iliyopita ya ligi kuu nchini Uingereza ikipokea kipigo kizito cha 5-0 nyumbani Old TRafford dhidi ya Liverpool.

Antonio Conte anatajwa ataenda kuwa mrithi endapo Solskjaer akifukuzwa.Conte amekuwa hapendi kuchukua timu katikati ya msimu lakini ukubwa na ndoto ya kuifundisha Man Utd ndiyo kitu pekee kinachoweza kumbadilisha mawazo yake.

Conte anaamini kwa kikosi cha sasa cha Man Utd anaweza kuipa timu hiyo mafanikio ndani ya msimu huu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka