Connect with us

Makala

Niyonzima Arejea As Kigali

Kiungo mshambuliaji wa zamani wa klabu za Simba sc na Yanga sc Haruna Niyonzima amerejea katika klabu ya As Kigali kama mchezaji huru kwa mara ya tangu tangu alipofanya hivyo mwaka 2019 na 2022.

Kiungo huyo Fundi raia wa Rwanda alicheza nchini katika klabu ya Yanga sc kwa miaka takribani nane kisha akajiunga na Simba sc ambapo hakudumu sana akarejea nchini kwa lo katika klabu ya As Kigali kisha akarudi Yanga sc kwa mkataba mfupi na kurudi tena As Kigali mwaka 2022.

Hata hivyo baada ya muda staa huyo alipata ofa katika klabu ya Al Ta’awon ya nchini Libya ambapo alidumu kwa siku 52 pekee na kuamua kuachana na klabu hiyo kutokana na kutofuata matakwa ya kimkataba.

As kigali itafaidika na ujio wa Niyonzima kutokana na uzoefu wake klabuni hapo ambapo sasa wanajiandaa na michezo ya nusu fainali ambapo sasa iko katika nafasi ya nne ikiwa na alama 23.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala