Connect with us

Makala

“Nitawafunga”Asisitiza Ateba

Mshambuliaji wa klabu ya Simba Sc Lionel Ateba ameahidi kuwapa furaha mashabiki wa klabu hiyo kuelekea mchezo wa ligi kuu ya Nbc nchini dhidi ya Klabu ya Yanga sc utakaofanyika Oktoba 19 jijini Dar es Salaam.

Ateba ameahidi kuwa siku hiyo lazima atafunga bao licha ya kuwa atakabwa na mabeki wazuri wakiongozwa na Ibrahim Hamad Bacca na Dickson Job ambao mpaka sasa hawajaruhusu kufungwa hata bao moja.

Mshambuliaji huyo ambaye Yanga sc ilikua na mpango wa kumsajili kabla ya kutua Simba sc amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika siku maalumu ya klabu huyo kuzungumza na vyombo vya habari kwa mujibu wa takwa la kikanuni la bodi ya ligi kuu nchini.

“Sitaki kujua Yanga wana Mabeki wazuri, sitaki kujua kuwa wana ulinzi mzuri, sitaki kujua wana Beki sijui anaitwa Sergio Ramos, kwanza sitaki hata kujua majina yao ila nina uhakika nitaingia uwanjani kwenye derby na nitawafunga Yanga na Simba tutashinda, sitaki kujua wana Beki wa aina gani”.Alisema Ateba kwa msisitizo

Klabu hizo zitamenyana katika mchezo huo unaotarajiwa kuwa wa kusisimua kutokana na upinzani baina yao huku Simba sc ikitarajiwa kutokubali kirahisi kupoteza mchezo huo baada ya kufungwa mara kadhaa mfululizo ikiwemo kipigo cha mabao 5-1 msimu uliopita katika mchezo wa kwanza huku ule wa raundi ya pili wakikubali tena kipigo cha mabao 2-1.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala