Connect with us

Soka

Ninja Awatema Yanga sc

Beki Abdallah Shaibu “Ninja”amesaini mkataba na timu ya klabu ya MFK Vyoskov inayoshiriki ligi daraja la tatu Jamhuri ya Czech wa miaka minne na kisha kutolewa kwa mkopo katika timu ya MFK la Galaxy ya Marekani.

Inasemekana beki huyo Mzanzibar tayari ameshasaini mkataba huo na muda wowote ataondoka nchini endapo taratibu za viza zikikamilika na kwenda nchini humo.

Mchezaji huyo ambaye alisajiliwa na Yanga miaka miwili iliyopita alitajwa kuwa mrithi wa nahodha msitaafu Nadir Haroub licha ya kukubwa na changamoto mbalimbali katika msimu wa kwanza ikiwemo kukosa nafasi ya moja kwa moja kikosini.

Inaripotiwa kwamba klabu ya Yanga bado imeendelea na juhudi za kumsaka mlinzi huyo ili kumuongezea mkataba wa kuendelea kukipiga klabuni hapo kama ripoti ya kocha Zahera inavyotaka.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka