Connect with us

Soka

Ngushi Atua Coastal Union

Mshambuliaji wa klabu ya Yanga sc Crispin Ngushi amejiunga na klabu ya Coastal Union kwa mkopo mpaka mwishoni mwa msimu huu baada ya kukosa nafasi katika kikosi cha kwanza cha klabu hiyo tangu asajiliwe akitokea Mbeya Kwanza.

Ngushi muda mfupi baada ya kusajiliwa aliumia kiasi cha kupelekwa nchini Afrika ya kusini kwa matibabu zaidi ambapo baada ya kurejea alihitaji muda kukaa sawa kutokana na kutokuwa na utimamu wa mwili.

Kocha Miguel Gamondi alianza msimu akiwa na matumaini makubwa na Ngushi hasa katika michuano ya ngao ya jamii mkoani Tanga ambapo alimpa nafasi mara kwa mara lakini mshambuliaji huyo alishindwa kuonyesha kiwango kizuri na kuanza kumuweka benchi.

Uwepo wa Pacome Zouzou,Kennedy Musonda na Clement Mzize kumechangia kwa kiasi kikubwa Ngushi kukosa nafasi huku mfumo wa kocha Gamondi wa kutotumia mawinga halisi ulisababisha staa huyo kukosa nafasi kikosini humo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka