Connect with us

Soka

Ndemla Atua Mtibwa Sugar

Klabu ya Mtibwa Sugar imemtambulisha rasmi kiungo Said Ndemla iliyemsajili kutoka Simba sc kwa mkataba wa mkopo wa msimu mzima wa ligi kuu wa 2021/2022.

Ndemla aliyekuzwa na klabu ya Simba sc ametolewa kwa mkopo kwa mapendekezo ya mwalimu Didier Gomes ambaye amesajili mastaa kadhaa kutoka baadhi ya timu za ndani na nje ya nchi hivyo hakuona haja ya kubaki na kiungo huyo kipenzi cha mashabiki wa klabu ya Simba sc.

Baadhi ya mastaa wamejiunga na Mtibwa Sugar wakiwemo Abdi Banda hivyo ujio wa Ndemla klabuni hapo utakwenda kuongeza ushindani katika mechi zaligi kuu msimu ujao.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka