Connect with us

Soka

Napoli 100%,Juve yamnyamazisha Mourinho Seria A

Mzunguko wa nane(8) wa ligi kuu ya soka nchini Italia(Seria A) huku klabu ya Napoli ikiendeleza ubabe mpaka sasa wakiwa na ushindi wa asilimia 100 baada ya kupata ushndi wa goli 1-0 dhidi ya Torino likifungwa na nahodha Lorenzo Insigne kwa mkwaju wa penati kuendelea kujikita kileleni mwa ligi hiyo.

Katika mchezo wa wiki kati ya Juventus dhidi ya AS Roma ya Jose Mourinho imewashuhudia Juve wakiondoka na ushindi mwembamba katika mchezo mkali uliofanyika katika dimba la Allianz Stadium Jijini Turin.

Licha ya kutawala mchezo kwa kiasi kikubwa As Roma hawakufanikiwa kuzigusa nyavu za Vibibi vizee hao wa Turin wakiongozwa na ukuta mgumu wa Bonucci na Chielini.

AC Milan walipata ushindi wa 3-2 dhidi ya Heras Verona huku mabingwa watetezi Inter Milan wakitandikwa 3-1 na Lazio ambao msimu huu wamekuwa wakitoa dozi kwa timu kubwa kwenye ligi hiyo.

Msimamo Seria A baada ya mzunguko wa nane;

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka