Connect with us

Makala

Mudathir,Feisal Matatani

Wachezaji Mudathir Yahaya wa klabu ya Yanga sc na Feisal Salumu wa klabu ya Azam Fc wako matatani kufungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya shilingi laki tano kila mmoja kutokana na kutoshiriki katika zoezi la kusalimiana na wachezaji wenzao pamoja na marefarii wa mchezo baina ya klabu zao siku ya jumatatu.

Wachezaji wakati wenzao wakisaliana kabla ya mchezo kuanza wenyewe kila mmoja alimtegea mwenzie kuingia uwanjani ambapo waliingia uwanjani baadae wakati wa kupiga picha za ukumbusho wa vikosi vyao.

Kwa mujibu wa kanuni kanuni ya 41:5 (5.4) kufanya kitendo chochote cha aibu, kama vile kukojoa kiwanjani, kukataa kupeana mkono na mgeni rasmi, waamuzi na wachezaji wa timu pinzani, kutoa au kuonesha ishara inayoashiria matusi.

Fei Toto alikuwa anafanya mazoezi ya viungo kwa kunyoosha miguu huku Mudathir akikung’uta viatu vyake ikionekana ni ujanja wa kila mmoja kumtegea mwenzake aanze kuingia uwanjani kitendo ambacho kanuni za ligi zinakitafsiri kama kutokuwa na uungwana lakini pia kikihusishwa na imani za kishirikina.

Mpaka sasa haijajulikana ni lini kamati hiyo itakaa kupitia ripoti mbalimbali za mwezi oktoba ambapo endapo itakaa mapema basi wachezaji hao wanaweza kuzikosa mechi za mwanzoni mwa mwezi novemba ambapo kwa Mudathir anaweza kuukosa mchezo dhidi ya Simba sc.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala