Connect with us

Soka

Mudathir Akabidhiwa Mamelod

Klabu ya Yanga sc imeamua mchezo wa hatua ya robo fainali ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika dhidi ya Mamelod Sundowns ya Afrika kusini kuikabidhi kwa jina la “Muda day” ikiwa ni moja ya njia ya kuenzi mchango wa mchezaji Mudathir Yahaya Abbas kikosini humo.

Yanga sc imekua na utaratibu wa kuipa thamani michezo yao mikubwa ikiwa ni njia ya kuongeza hamasa kikosini humo ambapo michezo hiyo hupewa jina la mchezaji mmoja wa kikosi cha kwanza cha klabu hiyo ili kumtia hamasa ya kuendelea kufanya vizuri ambapo michezo hiyo huambatana na kufanya kitendo fulani kuendana na staili ya muonekano wa mchezaji husika.

“Uongozi na benchi la ufundi wameazimia kwa pamoja kuwa mchezo wetu dhidi ya Mamelodi Sundowns, akabidhiwe kijana kutoka Kizimkazi, Mudathir Yahya. Slogani yetu kwenye mechi hii ‘SIMU ZIITE TUKUTANE KWA MKAPA’ Kazi ambayo tunayo kuanzia sasa hivi ni kupiga simu kwa watu wote tuwaambie tukutane kwa Mkapa”Alisema Ally Kamwe mkuu wa Idara ya Habari ya klabu ya Yanga sc.

Yanga sc itacheza mchezo huo siku ya jumamosi machi 30 saa tatu usiku katika uwanja wa Benjamini Mkapa ambapo itapaswa kushinda mchezo huo ili kujiwekea mazingira sahihi ya kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo mikubwa kwa ngazi za klabu barani Afrika.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka