Connect with us

Soka

Msuva Aikacha Yanga Sc,Atua Uarabuni

Mshambuliaji wa Kimataifa kutoka Tanzania Simon Msuva amekataa kurudi nyumbani kujiunga na klabu ya Yanga na kuamua kujiunga na klabu ya Al Najmah inayoshiriki Ligi Daraja la kwanza Saudi Arabia.

Kipindi cha dirisha dogo la usajili kulikuwa na tetesi za nyota huyo aliyewahi kutamba akiwa na Yanga anaweza akarejea kwenye timu hiyo mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara akiwa mchezaji huru baada ya kuvunjiwa mkataba na JS Kabylie ya Algeria.

Wakati wengi wakiamini anarudi Jangwani alikoondoka tangu msimu wa 2017/18 na kutua Difaa El Jadida, msuva hakurejea kucheza Ligi Kuu Bara na ameendelea kucheza nje ya nchi ikiwa ni mara ya pili anarudi Saudi Arabia kucheza Ligi Daraja la Kwanza.

Sasa tayari mshambuliaji huyo ametambulishwa katika klabu hiyo ambapo Baada ya utambulisho huo, kwenye akaunti ya klabu ya Instagram, Msuva aliongea akifurahia kujiunga na timu hiyo ambayo kwenye msimamo wa ligi hiyo, iko nafasi ya tisa baada ya kucheza michezo 18 na ina pointi 25.

“Nafurahia kusaini Al Najma, nafurahi kurudi Saudi Arabia na tutaonana baadaye,” alisema Msuva ambaye sasa atajiunga na klabu hiyo hivi karibuni baada ya Stars kutolewa katika michuano ya Afcon 2024.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka