Connect with us

Soka

Msudani Atua Biashara Utd

Timu ya Biashara United ya mkoani Mara imeendelea kuboresha kikosi chake kwa kusajili mchezaji Yassir Khemis Celestino kwa mkataba wa mwaka mmoja ili kusaidia timu hiyo iliyonusurika kushuka daraja katika msimu wa ligi kuu uliopita.

Beki huyo mwenye miaka 25 amesajiliwa akitokea timu ya Katori Fc inayoshiriki ligi kuu nchini Sudan na amefanikiwa kufunga mabao 5 katika ligi hiyo msimu uliopita.

Celestino pia ni mchezaji wa timu  ya taifa ya nchi hiyo akiwa amefanikiwa kucheza jumla ya michezo sita katika michuano mbalimbali.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka