Connect with us

Soka

Moroko Aikacha Mbao

Uongozi wa Klabu ya Mbao FC umekubaliana na kocha wao mkuu Hemed Suleiman Morocco kuvunja mkataba wa kuendelea kuifundisha klabu hiyo yenye makao yake makuu mkoani Mwanza.
Inasemekana chanzo cha kuvunja mkataba huo ni mfululizo wa matokeo yasiyoridhisha ya timu hiyo ambayo
kwa sasa inashika nafasi ya 18 kwenye msimamo ikiwa na alama 19 baada ya michezo 22 ya ligi kuu Tanzania bara.
Tangu Jana Kocha Morocco alithibitisha kwamba yeye na msaidizi wake Abdulmutik wameondoka jijini mwanza na sasa wako kwao Visiwani Zanzibar huku akisema pande zote mbili zimeachana kwa Amani baada ya kukubaliana kuvunja mkataba.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka