Connect with us

Soka

Morisson awashukuru rasmi Yanga

Licha ya kushinda kesi na kuwatambia mitandaoni kwa vijembe,mchezaji wa Simba Benard Morisson ni kama amekumbukua fadhila za waajiri wake hao wa zamani na kuamua kuwashukuru kwa ujumbe maalum.

Kupitia akaunti yake rasmi ya Instagram Morisson maarufu kama wakili msomi ameweka ujumbe wa kuwashukuru Yanga na mashabiki wake.

Aliandika ‘’kuna mwanzo na mwisho wa kila kitu,hakuna kinachodumu milele.Tumekuwa tukingojea uamuzi huu uwe mzuri au mbaya,hatimaye umefika na mwisho wa misukosuko yote.Nataka kila mtu ajue ni kiasi gani naishukuru Yanga kwa kunipa nafasi ya kuwatumikia na kuvaa nembo yao,hakuna mtu hapa Tanzania aliyenijua mpaka pale Luc Aymel aliponileta  kuja kucheza hapa,asante kocha kwa kuniamini na kunifanya kuwa bora.

Aliendelea ”kuna msemo Ghana kuwa mganga mbaya anayekuhudumia kabla ya kuja kwa mganga mzuri anapaswa kushukuriwa hata kama alikuwa mbaya,Niwashukuru rasmi Yanga na kila mmoja aliyenifanya nitabasamu na kunipenda bila kusahau upenda walionionesha mashabiki.HAKUNA KINACHOPATIKANA BILA KUPIGANIWA”.

Kitendo hicho cha Morisson kimepongezwa na wadau wa soka nchini kutokana na kuthamini mchango wa klabu kumfikisha alipo leo.

Morisson alishinda kesi dhidi ya rufaa ya Yanga katika mahakama ya usuluhishi wa michezo duniani CAS siku ya jana na CAS kuamuru wamlipe Tsh milioni 12 kama gharama za kesi.

Kwa upande wao Yanga walitoa taarifa ya kukubaliana na uamuzi huo na kuamua kusonga mbele,huku ikiwataka wanachama na mashabiki wake kuendelea kuiunga mkono timu kwenye harakati zake za kupigania taji la ligi kuu soka Tanzania Bara walilolikosa kwa miaka mine.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka