Connect with us

Soka

Molinga Kutua Morocco

Mshambuliaji wa Yanga sc David Molinga atajiunga na klabu ya RS Berkane inayoshiriki Ligi Kuu nchini Moro mara tu mkataba wake utakapomalizika mwishoni mwa msimu huu.

Kwa mujibu wa Taarifa za ndani Kocha wa zamani wa Yanga Mwinyi Zahera, anatajwa kuwa nyuma ya uhamisho wa straika huyo wa kimataifa wa Congo na ikumbukwe ndiye aliyemsaini klabuni hapo kabla ya kutimuliwa.
“Kila kitu kuhusu uhamisho tayari kimekwisha fanyika na sasa tunasubiri ni mkataba wake na Yanga kumalizika,” Zahera akizungumza na Gazeti la MwanaSpoti.

Licha ya kupigiwa kelele kuhusu kiwango chake na mashabiki wa klabu yake Hadi sasa msimu huu David Molinga ndio kinara wa mabao katika klabu ya Yanga, ameweka kambani mabao 10 kwenye Ligi ya VPL.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka