Connect with us

Makala

Mkude Ashindwa Kesi ya Metl

Kiungo wa klabu ya Yanga sc Jonas Mkude ameshindwa kesi aliyoifungua mahakamani dhidi ya Kampuni ya Mohamed Enterprises Limited akidai fidia ya kiasi cha bilioni moja kutokana na Kampuni hiyo kutumia picha zake katika mitandao yake ya kijamii.

Mkude alidai kuwa Julai 12 mwaka 2022 Kampuni hiyo iliposti picha zake akitangaza matangazo ya bidhaa za kampuni hiyo ilhali yeye hakua mchezaji wa klabu ya Simba Sc baada ya mkataba wake na klabu hiyo kumalizika.

Katika uamuzi wa kesi hiyo Mahakama imeipa ushindi kampuni ya Metl kwa baada ya kuthibitisha kuwa mchezaji huyo alikua aa mkataba na klabu ya Simba Sc mpaka Julai 30 2022 hivyo kampuni hiyo kutumia picha zake ilikua iko sahihi kwa mujibu wa Sheria.

Hivyo Hakimu pamoja na kuipa ushindi kampuni hiyo pia aliamuru Mkude kulipa gharama za kesi ambazo kampuni hiyo itakua imeingia katika kujibu mashtaka hayo.

Mkude ambaye mpaka sasa amecheza jumla ya mechi 34 za derby ya Simba Sc dhidi ya Yanga sc,alijiunga na klabu ya Yanga sc msimu wa 2022/2023 baada ya kumaliza mkataba katika klabu ya Simba Sc.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala