Connect with us

Soka

Mjipange,Deo Kanda Anarejea

Winga wa klabu ya Simba mkongo Deo Kanda amerejea nchini tayari kuanza kukitimikia kikosi cha wekundu hao baada ya kuwa nje kwa majeraha ya mguu.

Kanda aliyeumia Januari 4 kwenye mechi baina ya watani wa jadi Simba na Yanga alitolewa dakika ya 46 baada ya kufunga bao na kuumia baada ya kufanyiwa faulo na Juma Abdul.

Staa huyo alienda nchini Kongo ili kupata matibabu zaidi huku akiwa na familia yake na sasa amerejea mazoezini akisubiri maamuzi ya kocha kumchezesha.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka