Connect with us

Makala

Minziro Aikataa Penati ya Simba Sc

Kocha wa klabu ya Pamba Jiji ya jijini Mwanza Fred Felix Minziro ameikataa penati iliyopewa klabu ya Simba Sc katika mchezo wa ligi kuu baina ya timu hizo uliofanyika katika uwanja wa Ccm Kirumba jijini Mwanza na Simba sc kuibuka na ushindi wa 1-0.

Katika Mchezo huo Simba sc ilipata penati dakika ya 23 baada ya mshambuliaji Lionel Ateba kuangushwa wakati akimtazama kipa Yona Amos wa Pamba Jiji na mwamuzi kuamuru penati iliyoipatia Simba sc bao pekee kwenye mchezo huo.

Minziro alitoa maoni yake wakati wa mkutano na waandishi wa habari baada ya mchezo huo ambapo hakukubaliana na maamuzi hayo sambamba na kitendo cha mwamuzi kuongeza dakika mbili pekee ambazo alidai ni chache kutokana na mchezo ulivyokua unasimama kila muda.

“Sijui lakini kama ile ilikuwa ni penati, ligi yetu imekuwa bora, timu zinatumia gharama ila waamuzi wametuonea sana, wachezaji wao wamepoteza muda ila mwamuzi ameongeza dakika mbili alitakiwa aongoze dakika nane hadi kumi.”

“Simba kama wangekuwa wanaume kweli wangetufunga 5, nimeshangaa kwanini mwamuzi aliongeza dakika 2 wakati zilistahili kuwa 5 au 7, pia sina uhakika kama lile tukio lilistahili kuwa penati.”Alimalizia kusema kocha huyo mkongwe na mzawa hapa nchini.

Sambamba na kupoteza mchezo huo sasa Pamba Jiji imecheza jumla ya michezo 12 ya ligi kuu bila kuibuka na ushindi wowote huku wakiwa katika nafasi ya pili kutoka mkiani mwa ligi kuu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala