Connect with us

Soka

Messi atibuana na Pochettino

Mchezaji wa Paris St German Lionel Messi ameonekan kupishana kauli na kocha wake Mauricio Pochettino wakati akielekea kwenye benchi alipofanyiwa mabadiliko dakika ya 75 katika mchezo wa ligi ya Ufaransa dhidi ya Lyon.

Messi alionekana kukasirika mabadiliko hayo yalimuingiza uwanjani Achraf Hakim na hata alipokaa benchim alionekana kutokuwa na furaha hali inayozua hofu juu ya mahusiano yake na kocha huyo.

Katika mchez hu PSG walishinda magoli 2-1 yakifungwa na Neymar Jr dakika ya 66 kwa mkwaju wa penati na dakikka ya 90+3 kupitia Mauro Icardi na kuendelea kuongoza msimamo wa ligi hiyo.

Mgogoro huu wa kocha Pochettino ni muendelezo wa matukio ya mastaa wa timu kupishana kauli kila mara na makocha wa timu hiyo pale wanapoona hawaridhishwi na maamuzi ya wakufunzi wa timu hiyo hali inayopelekea kufukuzwa kwa makocha hao.

Messi mpaka sasa bado hajaifungiwa timu hiyo bao lolote licha kuanza michezo mitatu ya hivi karibuni.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka