Connect with us

Soka

Mcolombia Atambulishwa Azam Fc

Klabu ya soka ya Azam Fc imemtambulisha mshambuliaji Franklin Navarro raia wa Columbia mwenye miaka 24 ambaye amejiunga na klabu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili akitokea klabu ya Cortuluá ya nchini humo.

Usajili wa mshambuliaji huyo unaweka rekodi ya kuwa Mcolombia wa kwanza kucheza nchini ambapo anatarajiwa kuchukua nafasi ya Idriss Mbombo ambaye kwa mujibu wa taarifa za ndani ni kuwa anaweza kutemwa muda wowote klabuni hapo.

Azam Fc tayari imemtambulisha mshambuliaji huyo kupitia vyanzo rasmi vya taarifa vya klabu hiyo na tayari amejiunga na kambi ya timu hiyo iliyoko visiwani Zanzibar katika michuano ya kombe la Mapinduzi ambapo jioni hii wamecheza na Mlandege Fc na kutoa suluhu.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24, inaelezwa ni mtalamu wa kucheka na nyavu na ana kasi ya kukimbia huku akiwa na uwezo wa kucheza kama mshambuliaji wa kati ama pembeni.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka