Kamati ya Sheria na hadhi za wachezaji na wanachama ya TFF inakutana kesho Alhamisi tarehe 18 April 2024 kupitia mashauri tofauti tofauti ikiwemo sakata la mshambuliaji wa Azam FC PRINCE DUBE ambaye amaejiweka mbali na klabu hiyo akitaka kuondoka kwa madai mbalimbali yakiwemo ya kimkataba.
Habari ambazo Bin Kazumari inazo zinasema Dube aliiandikia TFF kulalamika kuhusiana na mkataba mpya wa Azam FC kwamba kuna vitu haviko sawa kwahiyo hautambui. Dube Ana mkataba na Azam FC ambao unaisha Julai 24 2024 na ndipo unapaswa kuanza mwingine wa miaka 2 mpaka Julai 2026.
Katika kesi hiyo itakayoanza kesho Alhamisi tarehe 18 April 2024 Azam FC watawakilishwa na wakili wa kimataifa kutoka Ureno na ameshawasiliana na TFF kuona uwezekano wa shauri la Prince Dube kufanyika kwa njia ya mtandao (zoom meeting) ili aweze kushiriki akiwa huko huko Ureno.
Kwa upande wa mshambuliaji Prince Dube mpaka sasa bado haijajulikana kuwa watetezi wake watatoka upande upi kama ni nje ya nchi ama humuhumu ndani.
Dube ana mgogoro wa kimkataba na klabu yake ya Azam Fc ambapo pamoja na klabu hiyo kupokea ofa kadhaa za kumuuza bado mshambuliaji huyo amesisitiza kuondoka klabuni hapo kwa kuvunja uliopo huku akigoma kuutambua mkataba mpya aliousani hivi karibuni utakaomuweka klabuni hapo mpaka 2026.
Cc:Jemedari Saidi