Connect with us

Soka

Mbao Wagoma Kuingia Kambini

Licha ya uongozi wa klabu ya Mbao fc kuwaita wachezaji wake kambini kujiandaa na michezo ya ligi kuu iliyosalia taarifa zkutoka klabuni hapo zinadai hakuna mchezaji hata mmoja aliyeripoti kambini.

Klabu hiyo wenyeji wa jiji la Mwanza maeneo ya sabasaba wameiomba bodi ya ligi (TPLB) na Shirikisho la soka Tanzania (TFF) kuikopesha pesa klabu hiyo ili iweze kumudu gharama za kuiweka kambi timu jijini Dar es salaam kumalizia michezo iliyosalia.

Awali serikali kupitia kwa Waziri mwenye dhamana ya Michezo nchini Dk.Harrison Mwakyembe aliweka wazi kuwa michezo yote iliyosalia ya ligi kuu itachezwa jijini Dar es salaam ili kuepuka maambukizi ya Virusi vya Corona ambapo timu zitapaswa kuweka kambi katika jiji hilo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka