Connect with us

Soka

Mbao Kuwavaa Coastal Kirumba

Klabu ya Mbao FC ikiwa kwenye presha ya kushuka daraja leo inakutana na Coastal Union mchezo utakaopigwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba  jijini Mwanza.

Mbao ambayo imecheza mechi 30 hadi sasa imeshinda mechi 5, sare 8 na kupoteza michezo 17 inahitaji kupata ushindi kwenye mechi zake zilizobaki ili ijinusuru isishuke ligi kuu.

Timu hiyo tayari imeshabadili kocha kwa kumuondoa Abdulmutik na kumchukua Felix Minziro (bingwa wa kupandisha timu kutoka daraja la kwanza kwenda ligi kuu).

Minziro anasema: Naiheshimu Coastal Union ni timu nzuri na imefanya usajili mzuri msimu huu ndio maana kwenye ligi wapo katika nafasi nzuri sisi tupo chini.”

“Tunaingia kupambana kutafuta pointi 3 hakuna kingine kwa sababu tupo chini kwenye msimamo wa ligi, hakuna kingine zaidi ya kutafuta ushindi.”

Mbao inakutana na Coastal union iliyochini ya Juma Mgunda ambaye msimu huu kwake umekuwa bora sana akiwa na Wagosi wa kaya akiwa kwenye nafasi salama, ina pointi 48 baada ya kucheza mechi 30, inashika nafasi ya 5 kwenye msimamo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka