Connect with us

Soka

Mazembe Yawafata Fei Toto,Tshabalala

Mabingwa mara tano wa Afrika klabu ya Tp Mazembe ya Kongo wako nchini toka katikati ya wiki hii kwa lengo moja tu la kuwanasa kiungo mjanjamjanja wa Yanga Feisal Salum Abdalah ‘Fei Toto’ na beki wa kushoto wa Simba Sc Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ kwa ajili ya kuwasainisha mikataba wajiunge na klabu hiyo.

Hata hivyo klabu hiyo itakutana na wakati mgumu kuwanasa wachezaji hao kwa kuwa wote wana mikataba na klabu zao hasa Mohamed Hussein ambaye ambaye alisaini mkataba mpya na wekundu wa Msimbazi Simba sc hivi karibuni.

Pia klabu hiyo ya Kongo ipo kwenye mazungumzo na wazazi wa mshambualiaji wa Serengeti Boys Kelvin John ‘Mbappe’ kwenda kujiunga na Timu hiyo huku wakiwa tayari kumsomesha kinda huyo.

Mazembe hivi karibuni ilikamilisha usjili wa mshambuliaji wa Mbeya city Eliud Ambokile kwa mkataba wa miaka mitatu na nusu siku kadhaa baada ya kushindwa kumsajili Ibrahim Ajibu Baada ya kushindwana maslahi binafsi na mchezaji huyo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka