Connect with us

Makala

Matampi Ampiku Diarra

Golikipa wa klabu ya Coastal Union Ley Matampi amempiku golikipa wa klabu ya Yanga Djigui Diarra na kuwa kipa mwenye clean sheets nyingi baada ya kufikisha 15 huku Diarra ambaye hakucheza mechi ya leo dhidi ya Tanzania Prisons akibakiwa nazo 14.

Matampi ambaye hakua na mwanzo mzuri alipojiunga na Coastal Union akitokea nchini Congo Dr ambapo baada ya muda alirejea katika kiwango chake huku kocha David Ouma raia wa Kenya akionyesha kumuamini na kumpa nafasi mara kwa mara kikosini humo.

Kipa huyo amempa changamoto Diara ambaye alitwaa tuzo hiyo mara mbili katika misimu miwili iliyopita ambapo kwa msimu huu amecheza jumla ya michezo 21 na kupata cleen sheet 14 huku Matampi akipata 15 katika michezo 24 ya ligi kuu nchini.

Kipa huyo kutokana na kiwango hicho tayari baadhi ya vilabu vimeanza kumvizia kumsajili hususani klabu ya Simba sc ambayo imeonyesha nia ya kumsajili kuchukua nafasi ya Ayoub Lakred ambaye ana mpango wa kutoongeza mkataba katika klabu hiyo baada ya kupata ofa nono katika nchi za kaskazini.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala