Connect with us

Soka

Mastaa Yanga sc Wavuna 700m

Baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 5-1 mastaa wa klabu ya Yanga sc wamefanikiwa kupata bonasi ya kiasi cha shilingi milioni mia saba kutoka kwa uongozi wa klabu hiyo chini ya Rais Eng.Hersi Said na ufadhili wa bosi Gharib Said Mohamed.

Awali kabla ya mchezo huo mabosi hao waliwaahidi wachezaji hao kuwa kila goli moja watanunua kwa kiasi cha shilingi milioni mia moja kwa mechi ambayo watashinda ambapo baada ya kupata ushindi huo mabosi hao waliamua kuongeza tena shilingi milioni mia mbili zaidi.

Kutokana na mamilioni hayo sasa inasemekana kila staa wa kikosi hicho ana uhakika wa kukunja milioni 15 kama bonasi kutokana na ushindi huo huku bonasi hizo zikiendelea katika kila mchezo kulingana na uzito wa mechi husika.

Yanga sc ilipambana kuifunga Simba sc ili kupunguza pengo la alama tatu ambalo kama Simba sc angeshinda basi angewazidi alama sita mabingwa hao wa msimu uliopita wa ligi kuu nchini.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka