Connect with us

Makala

Mastaa Waitwa Stars Kuivaa Dr Congo

Kocha Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Hemed Morocco ametaja kikosi cha mastaa mbalimbali wa ndani na nje ya nchi kujiunga na kambi ya timu hiyo kwa ajili ya michezo miwili ya kuwania kufuzu michuano ya mataifa ya Afrika mwaka 2025 dhidi ya Dr Congo.

Michezo hiyo miwili inatarajiwa kufanyika Oktoba 10 na 15 mwaka huu ugenini na kisha kumalizia nyumbani katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Katika kikosi hicho makipa Yona Amos wa Pamba Jiji,Ally Salim wa Simba sc n Zubeiry Foba wa Azam Fc ndio wameitwa wakiungana na mastaa wengine kama inavyoonekana pichani.

Mshambuliaji mkongwe Mbwana Samata amerejeshwa kikosini baada ya kuombwa kusitisha Ombi lake la kustaafu kuichezea timu hiyo.

Kutoka Yanga sc kocha huyo ameamua kumuacha kipa AbouTwalib Mshery na beki Nickson Kibabage na kuwaingiza Zubeiry Foba na Abdulrazak Hamza ambao hawakuwepo mara ya mwisho.

Pia kocha huyo amemrejesha kikosini beki Haji Mnoga wa timu ya Salford City huku akimuita kwa mara ya kwanza mshambuliaji wa Fountain Gate Fc Seleman Mwalimu mwenye mabao matano ya ligi kuu katika michezo saba.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala