Connect with us

Soka

Mastaa Afcon Kuoga Noti

Rais wa Ivory Coast, Alassane Ouattara na Rais wa Nigeria, Bola Tinubu wametoa zawadi kwa wachezaji wa timu zao za Taifa ambazo zilicheza Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika iliyomalizika siku ya Februari 11 nchini Ivory Coast.

Baada ya wenyeji wa michuano hiyo timu ya Ivory Coast kuibuka mabingwa wa michuano hiyo kwa kuifunga Nigeria 2-1 ambapo wamepata kiasi cha fedha za kitanzania shilingi bilioni 17 kama zawadi ambapo Rais wa nchi hiyo ameahidi kuwapa kiasi cha 208 kwa kila mchezaji mbali na zawadi za Caf.

Washindi wa pili Nigeria wenyewe Rais wao Bola Tinubu yeye ametoa zawadi ya viwanja na nyumba kwa mastaa wa timu hiyo sambamba na tuzo ya heshima kwa kila mchezaji wa timu hiyo ambapo zawadi hizo ni nje ya shilingi bilioni 10 watakazopata kama zawadi.

Pia, Vyombo vya Habari vya Afrika Kusini vimedai Chama cha Soka cha Taifa hilo (SAFA) kinatarajia kutoa Dola za Marekani 52,000 (Tsh. Milioni 132) kwa kila Mchezaji wa Taifa kwa kushika nafasi ya Tatu katika michuano hiyo.

Timu zingine zilizoingia nusu fainali ni Congo DR na Afrika kusini ambazo zimepata zawadi ya shilingi bilioni 6.3 kutoka Caf huku zilizoingia hatua ya robo fainali zikipata shilingi bilioni 3.3 ambazo ni Angola,Guinnea,Mali na Cape Verde.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka