Connect with us

Soka

Mapinduzi ya Kijeshi Yaaharisha Mechi Guinnea

Shirikisho la Soka la Dunia (FIFA) na lile la Afrka (CAF) wamekubaliana kuhairisha mechi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia Kanda ya Afrika kati ya timu ya taifa ya Guinnea na Morroco mechi ambayo ilikuwa ichezwe leo Jumatatu pale Mjini Bissau.

Hii ni kutokana na mapinduzi ya Serikali ya Rais ALPHA CONDE yaliyofanywa na jeshi la nchi hiyo hapo jana ambapo ilisababisha Wachezaji na viongozi wa timu ya Taifa ya Morocco kusindikizwa Airport na Wanajeshi ili kuondoka nchini humo wakiwa salama.

Imeripotiwa kwamba milio ya bunduki imesikika katika baadhi ya mitaa nchini humo hasa mtaa wa Conakry ambao ndipo mechi ilikua ichezwe huku Fifa katika taarifa yake wamethibitisha kuahirisha mchezo huo kutokana na sababu za kiusalama zaidi huku wakisema watapanga siku nyingine kwa ajili ya mchezo huo wa kufuzu kombe la dunia.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka