Shirikisho la soka nchini Tanzania (TFF) limetangaza majina ya wachezaji 35 ambao wataingia kambini katika kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania kwa ajili ya michezo miwili ya kuwania kufuzu kombe la dunia dhidi ya Niger na Morocco.
Michezo hiyo inatarajiwa kuchezwa mwezi huu wa Novemba ambapo katika kikosi hicho mastaa Feisal Salum wa Azam Fc na Aishi Manula wa Simba sc wamerejea kikosini baada ya muda mrefu kupita tangu waitwe kwa mara ya mwisho.

Feisal alikua haitwi kutokana na kutokua fiti baada ya kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu alipokua na mgogoro na klabu yake ya Yanga sc ambapo mara ya mwisho kuitwa ilikua machi 28 mwaka huu siku ya mchezo dhidi ya Uganda wa kuwania kufuzu Afcon ambapo Stars ilikubali kipigo cha 1-0.
Kwa upande wa Manula yeye alikua na takribani miezi saba akiwa nje ya uwanja baada ya kufanyiwa upasuaji wa mguu na hivyo kuhitaji kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu zaidi ambapo amerejea hivi karibuni akicheza mchezo wake wa kwanza mkubwa dhidi ya Yanga sc katika kipigo cha mabao 5-1.
Mastaa wengine wapya katika kikosi hicho cha kocha Adel Amrouche ni kipa AbuuTwalib Mshery na Kwesi Kawawa anayecheza ligi nchini Sweden,Matheo Anthony wa Mtibwa Sugar,Edwin Balua wa Tanzania Prison,AbdulMalick Zakaria wa Namungo Fc na kiungo Ladack Chasambi wa Mtibwa Sugar.