Connect with us

Makala

Manula Atemwa Simba Sc Ikiifuata Bravos

Kipa Aishi Manula ametemwa katika msafara wa kikosi cha timu ya Simba sc kilichoondoka mapema leo kuelekea nchini Angola kuivaa klabu ya Bravos do Marquiz ya nchini humo katika mchezo wa marudiano wa hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho barani Afrika.

Katika msafara huo wa wachezaji 22 jina la Manula halimo huku mpaka sasa hakuna sababu iliyotolewa na uongozi wa klabu hiyo ambapo makipa Moussa Camara,Ally Salim na Hussein Abel ndio wameondoka na kikosi.

Maisha ya Manula katika klabu ya Simba Sc yamekua na wakati mgumu tangu aliporuhusu bap 5-1 kutoka kwa Yanga sc katika mchezo wa ligi kuu mwanzoni mwa mwaka jana.

Simba sc itawavaa Bravos katika mchezo muhimu ambao inapaswa kushinda ili kufuzu moja kwa moja hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala